Wednesday, November 13, 2013

HIFADHI YA MAZINGIRA

MTANDAO WA ASASI ZISIZO ZA KISERIKALI WILAYANI NKASI (NKANGONET) ULIVYOWEZESHA KIJIJI CHA SINTALI

 KUTUNZA MAZINGIRA KWA KUVILINDA VYANZO VYA MAJI NA MISITU YA ASILI

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Sintali wilayani Nkasi Sezari Katelema akionesha namna chanzo cha maji kilichopo jirani na shule hiyo kinavyotunza ili kiwe endelevu.Chanzo hicho hutiririsha maji kwa kipindi cha mwaka mzima pasipo kukauka lakini kilikuwa hatarini kutokana na uharibifu wa mazingira uliokuwa umeanza kufanyika kabla ya wakazi wa kata ya Sintali kupewa elimu ya utunzaji mazingira. Mwanamke mkazi wa kijiji cha Sintali wilayani Nkasi mkoani Rukwa,Happy Shilingi akiteka maji katika kisima kilichopo kwenye chanzo cha maji jirani na shule ya msingi Sintali.Utunzaji wa mazingira unaofanywa hivi sasa na wakazi wa kijiji hicho unatoa mwelekeo mzuri wa chanzo hicho ambacho hutiririsha maji kwa mwaka mzima kuwa endelevu. Msitu wa asili uliotengwa na kijiji cha Sintali wilayani Nkasi mkoani Rukwa ambao kutokana na elimu ya utunzaji wa Mazingira waliyoipata wakazi wa kijiji hicho na vijiji vingine vya kata ya Sintali mwaka huu haujachomwa moto na mikakati ya utunzaji baada ya elimu hiyo imeanza kuonekana kuwa yenye tija tofauti na miaka ya nyuma.Mtandao wa asasi zisizo za kiserikali wilayani Nkasi(Nkangonet) ndiyo ulitoa elimu hiyo kupitia mdahalo uliofanyika mapema mwaka huu kwa ufadhili wa The Foundation For Civil Society.
HABARI HII NI KW HISANI YA Joachim Nyambo

No comments: