TFDA ibomolewe, isukwe upya, wahujumu wa madawa ya umma washitakiwe.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MSIMAMO WA JUMUIYA YA VIJANA KWA TFDA NA WAUZAJI WA MADAWA YA
KULEVYA NCHINI.
·
·
Vinara wa Madawa ya kulevya nao watajwe na
kufikishwa mahakamani.
Serikali ya Tanzania kupitia wizara ya Afya, Mamlaka ya
Chakula na Dawa, pamoja na Mamlaka ya Bandari vimekuwa mawakala wakubwa wa
biashara haramu ya afya za watanzania. Afya za watanzania zinaendelea kuwekwa
rehani na waliopewa mamlaka ya kuongoza.
Wizara ya Afya imekuwa ikiruhusu uwepo wa zahanati na maduka
ya madawa yasiyo na wataalamu wa afya ambapo watanzania wengi wamekuwa wakipewa
dawa zisiendana na magonjwa wanayoumwa. Hali imesababisha madhara makubwa kwa
wagonjwa. Utafiti uliofanywa na Youth Initiative Tanzania (yiTa) na TWAWEZA
kuanzia Novemba 2011 hadi Agosti 2012 ulibaini kuwa zaidi ya 93% ya huduma
zinazotolewa katika zahanati na maduka binafsi ya dawa jijini Dar es salaam,
hutolewa bila kutumia utaalamu wa afya. Je, wizara ya Afya ina mpango gani wa
kukomesha hali hii?.
Pamoja na hali kuwa mbaya kiasi hicho, TFDA imekuwa ikpata
kashfa kubwa za kuhatariasha maisha ya watu kila kukicha lakini hakuna hatua
zozote zinazochukuliwa dhidi ya mabosi wa TFDA. Watanzania watakumbuka kuwa
mwishoni mwa mwaka 2011 watafiti wa ugonjwa wa Maralia toka Uingereza
wakiongozwa na Dr. Washington walitoa ripoti juu namna ambavyo Serikali za
Afrika zimekuwa zikipokea madawa bandia toka China na namna ambavyo madawa hayo
yanavyoathiri afya za watu. Lakin cha ajabu TFDA ilikana kupokea madawa bandia,
lakini baada ya miezi miwili madawa bandia ya Maralia yakakamatwa Mwanza na
Kilimanjaro. Ndipo baadaye viongozi wa TFDA walipojitokeza kwa aibu na kukiri
kuwapo kwa madawa hayo bandia nchini. Lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa
dhidi yao.
Hivi karibuni, kumepatika dawa feki za kuongeza nguvu za
waathirika wa VVU, lakini pia hakuna hatua zozote zilizokwisha chukuliwa.
Na cha kusikitisha zaidi, ni pale Watanzania wanaambiwa kuwa
hakuna dawa katika hospitali za umma wakati hospitali za binafsi zina shehena
ya dawa zilizoandikwa “NOT FOR SALE”. Na cha ajabu zaidi TFDA wanakili kuwa
wameibiwa dawa zilizotakiwa zitolewe bure kwenye zahanati na hospitali za
serikali lakini zimepotea na zinapatikana katika hospitali na maduka binafsi ya
dawa zikiwa zimefutwa nembo ya NOT FOR SALE. Wakati haya yanatendeka, hospitali
za umma ziko taabani, hakuna dawa. Imebaki kwenda hospitali na kupima, kisha
unaambiwa nenda ukanunue dawa katika dawa Fulani. Lakini serikali imekaa kimya
dhiti ya mamlaka hizi.
Jumuiya ya Vijana ya CUF (JUVICUF), inatambua kuwa endapo
hatua za haraka hazitachukuliwa, kunahatri kubwa ya kuwapoteza watoto wengi
ambao ndio vijana wa kesho. Akina mama na Vijana nao wako hatarini kupotea.
Hivyo tunaitaka serikali kuwaachisha kazi wakurugenzi wote wa TFDA ili hatua za
kisheria zichukue mkondo wake.
Nalo suala la watuhumiwa wa madawa ya kulevya limewekwa
kwapuni kwa sasa. Serikali ilishahidi kutoa orodha yao lakini haitaki kutoa
hadi sasa. Hili ni suala linaloathiri maisha na nguvu kazi ya vijana moja kwa
moja. Vijana wengi wanapotea kwa kuathirika na madawa ya kulevya.
JUVICUF inaitaka serikali iwataje wauzaji na wasambazaji wa
madawa ya kulevya nchini bila kujali vyeo na haiba yao katika jamii. Na baada
ya kuwataja, wafikishwe mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.
Endapo serikali haitachukua hatua za kuisafisha TFDA na
kuwataja pamoja na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa madawa ya kulevya kama
ilivyoahidi, na kwa kuwa waathirika wakubwa madawa ya Kulevya na madhara ya
kuuzwa kwa dawa kiholela pamoja hospitali za umma kukosa dawa ni Vijana,
JUVICUF itafanya maandamano ya amani hadi wizara ya afya kushinikiza hatua za
uwajibikaji na kisheria zichukuliwe.
Imeandaliwa na:
Thomas D.C Malima
Naibu Katibu
Jumuiya ya Vijana ya CUF (JUVICUF)-Taifa.
MATAMKO HAYO YANAJENGA AU KULINGANISHAJE NA HABARI HII KATIKA MAMLAKA NYETI KWA UHAI KAMA HII, SOMA HII YA FEBRUARY MWAKA HUU..........
Dawa feki za malaria zaingizwa nchini
25th February 2012
Mamalaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA)
Dawa hiyo imebainika kuwa ni
bandia, kutokana na maelezo yaliyopo katika lebo kuonyesha imetengenezwa
na kiwanda cha Elys Chemical Industries Ltd cha nchini Kenya, wakati
kiwanda hicho hakitengenezi dawa yenye jina la biashara la ‘Eloquine’.
Mkurugenzi
Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo, alisema kupitia taarifa yake kwa vyombo vya
habari jana kuwa, hadi sasa jumla ya makopo 155 ya dawa hiyo bandia
yaliyokuwa yakisubiri kusambazwa, yamekamatwa jijini Dar es Salaam.
Alisema kati ya makopo hayo, moja lenye vidonge 115 lilikamatwa mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Pia
mtuhumiwa mmoja amefikishwa mahakamani na upelelezi wa chanzo na
wasambazaji wa dawa hiyo unaendelea kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.
Alisema kiwanda cha Elys Chemical Industries Ltd kimesajili dawa ya Quinine Sulphate 300mg B.P isiyo na jina la kibiashara.
Sillo alisema kiwanda hicho kimebainisha tofauti mbalimbali zilizopo katika lebo ya dawa bandia ikilinganishwa na dawa halisi.
Dawa
halisi ya ‘Eloquine’ hutengenezwa na Elys Chemical Industries Ltd na
imesajiliwa na TFDA na hivyo kuthibitisha kuwa kiwanda hicho
hakitengenezi dawa hiyo bandia.
Alisema
uchunguzi wa dawa bandia katika maabara umebaini kuwa vidonge hivyo
havina kiambato hai kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa Malaria na hivyo
matumizi yake ni hatari kwa afya ya binadamu.
Mkurugenzi Mkuu huyo wa TFDA alisema pia maelezo ya kina yanatofautisha dawa halisi iliyosajiliwa na dawa bandia.
Alisema
kwa mfano, jina la dawa halisi iliyosajiliwa linasomeka: ‘Quinine
Sulphate 300mg B.P’, tofauti na lile la dawa bandia ambalo linasomeka:
‘Quinine Sulphate 300mg U.S.P’.
Tofauti
nyingine ni dawa halisi iliyosajiliwa kutokuwa na jina la biashara,
wakati dawa bandia ikiwa na jina la biashara la ‘ELOQUINE’.
Pia rangi ya lebo ya dawa halisi ni nyeupe na kahawia, wakati lebo ya dawa bandia ni ya rangi ya njano na nyekundu.
Tofauti nyingine inahusu muda wa matumizi, ambapo dawa halisi iliyosajiliwa ni miaka minne wakati dawa bandia ni miaka mitano.
Vilevile, namba ya toleo la dawa halisi iliyosajiliwa huanzia na namba, lakini dawa bandia huanzia na herufi.
“Kwa
mfano, namba ya toleo ya dawa halisi iliyosajiliwa inaanzia ‘2167E’,
namba ya toleo ya dawa bandia inaanzia ‘GE410’,” alisema.
Alisema
katika kuwakanganya watu zaidi, anuani ya mtengenezaji wa dawa bandia
imetumiwa ileile ya mtengenezaji wa dawa halisi iliyosajiliwa.
Anuani hiyo ni: Elys Chemical Industries Ltd, Road B, Off Enterprise Road, P.O. Box 40411, 00100 Nairobi, Kenya.
Kutokana na hilo, amewatahadharisha wafanyabiashara wote wa dawa na wananchi kutozitumia dawa hizo bandia.
Pia
amewaelekeza wale wote waliouziwa dawa hizo bandia kuzirudisha katika
ofisi za TFDA, vituo vya afya vya serikali au vituo vya polisi vilivyo
jirani nao.
Vilevile,
amewakumbusha wafanyabiashara wa dawa, wasafirishaji wa vifurushi na
wananchi kwa jumla, kutoa taarifa haraka iwezekanavyo pale wanapohisi
kuuziwa dawa duni, bandia au zilizoisha muda wa matumizi.
“Taarifa
zitolewe ofisi za TFDA makao makuu zilizopo Barabara ya Mandela, EPI
Mabibo External, Dar es Salaam na Ofisi za Kanda zilizopo mtaa wa
Nkurumah, Mwanza, Mtaa wa Sakina – Arusha, Hosptali ya mkoa wa Dodoma na
Jengo la Ofisi ya Mifugo Mkoa wa Mbeya,” alisema Sillo.
Msemaji
wa TFDA, Gaudensia Simwanza, alisema aliyefikishwa mahakamani,
ameshtakiwa kwa mujibu wa sheria namba 1 ya mwaka 2003 ya TFDA. Alisema
mtu huyo anatuhumiwa kukutwa akiuza dawa ambayo haijasajiliwa na TFDA
ambayo pia ni bandia.
Simwanza
alisema sheria hiyo haizungumzii dhamana, bali inazungumzia adhabu kwa
yeyote anayepatikana na hatia; ikiwamo kutozwa faini, kutumikia kifungo
jela au yote mawili kwa pamoja.
“Dhamana ni haki ya mtu, sababu yawezekana mtu akakutwa anauza dawa bandia bila kujua kuwa ni dawa bandia.
Tunachokifanya sisi (TFDA) ni kupeleleza kujua amenunua wapi dawa hiyo,” alisema Simwanza.
SOURCE:
NIPASHE
Wanahabari wakiwa katika mafunzo ya uandishi wa habari za afya
HOSPITALI
ya mkoa wa Iringa ilivyojipanga kukabiliana na tatizo la upatikanaji wa damu
salama kupitia mpango wa Taifa wa
damu salama.
Ikumbukwe kuwa damu ni moja kati ya mahitaji muhimu katika mwili wa binadamu awaye yeyote ili aweze kuishi ni lazima kuwa na damu ya kutosha mwilini mwaka.Hospitali na vituo vya afya vya umma na binafsi ila bado uelewa wa baadhi ya wananchi katika kujitolea kutoa damu limekuwa ni tatizo kubwa kutokana na jamii kutokuwa na utamaduni wa kufika katika banki za damu kwa ajili ya kutoa mchango wa damu.
Tayari serikali
kupitia wizara ya afya na ustawi
wa jamii imekwisha toa mwongozo wa damu
salama kama njia ya kujipanga kuboresha
huduma hiyo .
Lengo la
kutoa mwongozo kwenye uundwaji wa kupangwa vizuri huduma kuongezewa damu,
sambamba na Azimio la Afya Duniani Bunge WHA 28.72 (iliyopitishwa Mei 19,
1975) kwamba linataka nchi wanachama wote wa kuendeleza uratibu wa kuongezewa damu ni huduma ya msingi
na hiari
Pia kupangwa
vizuri Damu (BTS) ni sehemu muhimu ya mfumo wowote wa afya kujifungua ili kufanikisha mpango huo mkakati madhubuti kwa ajili ya
Usalama wa Damu inahitajika
Kutoka
2003 hadi 2007, Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Marekani imefanya ukarabati wa vituo 7 vya
kanda ambapo shughuli za mpango wa damu
salama umetekelezwa.
Vituo
hivi kanda (ZC) ambayo ni ya kijiografia aitwaye ni Ziwa (Mwanza), Kaskazini
(Moshi), Magharibi (Tabora), Mashariki (Tabora), Kusini (Mtwara), na nyanda za juu Kusini (Mbeya) na Zanzibar.
Meneja wa maabara ya mkoa wa Iringa Kimea
Myefu amesema kuwa katika kutekeleza mpango huo na kuona kuwa Hospitali ya mkoa wa Iringa haipungukiwi na akiba ya damu salama katika benki yake imekuwa na mpango
maalum wa kupata damu salama kwa kutenga bajeti maalum ya kusafirisha damu
kutoka Mbeya .
Myefu amesema
kuwa kutokana na mpango makakati
huo wa
kutenga bajeti ya kusafirisha damu
kwa kiasi tatizo la damu katika
benki ya damu salama Hospitali ya
mkoa kutokuwa tatizo sana.
Hata hivyo amesema
kuwa mwamuko kwa jamii katika
kujitolea damu katika mkoa
wa Iringa umekuwa mkubwa
zaidi ukilinganisha na miaka ya
nyuma kabla ya kuanzishwa mpango huo wa
damu salama .
Myefu
amesema kuwa idadi kubwa ya
wananchi wanaofika kuchangia damu
tayari wana elimu juu ya mpango huo na wanajua afya zao ila wale
wasiojua afya zao ndio wamekuwa
nyuma kujitokeza kuchangia damu.
“Kwa sasa idadi kubwa ya watu
wanaojitokeza kuchangia damu
zao wamekuwa wakichangia damu ila idadi ndogo hasa wale ambao ni
wageni kabisa katika kuchangia
damu ndio ambao wamekuwa wakiondoka bila kuchangia damu
kutokana na kutokuwa na uhakika
wa afya zao”amesema Myefu
Kuwa imeendelea
kutolewa na wananchi wengi wamekuwa wakijitokeza
kuchangia damu na kati ya watu
10 wanaofika kutoa damu ni wawili
ama mmoja pekee ndie ambae amekuwa akirudi pasipo kuchangia damu kutokana na
matatizo ya kiafya.
Aidha
amesema kuwa kuna haja ya jamii kujenga
utamaduni wa kuchunguza afya zao mara kwa mara ili pale ambapo
mchango wao wa damu utahitajika
basi kuweza kufika katika katika benki za damu na
kuchangia damu.
Akielezea
kuhusu utaratibu wa mchangiaji wa damu Myefu amesema kuwa kwanza ni lazima kupimwa H.I.V , homa ya ini , magonjwa ya
zinaa kama kaswende na mengine ,kiasi
cha damu alichonacho mchangiaji pamoja na matatizo ya presha ,Kwani
amesema kitaalam mwenye kuchangia damu
ni lazima awe na uzito wa kuanzia kilo 50 na kuendelea.
Akielezea kuhusu mahitaji ya kawaida ya damu katika
Hospitali hiyo ya mkoa kwa siku
kuwa ni uniti 8 na kuendelea
wakati akiba ya damu iliyopo
kwa sasa ni uniti 25 ambacho bado kidogo
ukilinganisha na mahitaji halisi ya
siku.
Hivyo
ameiomba jamii kujenga utamaduni wa kujitolea
kuchangia damu mara kwa mara ili
kuboresha zaidi huduma
hiyo .
Myefu
amesema kuwa baadhi ya wananchi
wanaofika kuchangia damu kwa ajili ya wagonjwa
wao wamekuwa wakiamini kuwa damu wanayochangia ni kwa ajili ya matumizi ya wagonjwa wao jambo ambalo halina ukweli wowote.
“Kimsingi
kama kuna mgonjwa anahitaji damu na ndugu
wakajitolea kuchangia damu damu hiyo haiwezi kutumika kwa wakati huo kwa ajili ya mgonjwa wake isipokuwa
atapewa damu nyingine ambayo imetoka kituo cha damu salama cha kanda kilichopo mkoa wa Mbeya na si vinginevyo”
Kwani
amesema kuwa damu inayochangiwa na katika Hospitali ya mkoa haitumiki hadi
ipelekwe katika kituo cha kanda kwa ajili ya kuihakiki ubora wake.
Pia
amesema kuwa damu imekuwa na matumizi makubwa
hasa pale inapotokea ajali na majeruhi kufikishwa katika hospitali hiyo.
Myefu
amesema kwa mchangiaji wa damu hakuna malipo
yoyote zaidi ya kupongeza kwa neon
la ahsante na kuwa hakuna biashara ya
damu inayofanyika katika Hospitali hiyo.
Wakati
Hospitali hiyo ya mkoa wa Iringa ikiwa na mkakati huo wa kuboresha zaidi
mpango huo wa damu salama uchunguzi
uliofanywa na wanahabari wanachama
wa klabu ya waandishi wa habari
mkoa wa Iringa (IPC) wanaopatiwa mafunzo ya uandishi wa habari za
afya chini ya ufadhili wa umoja wa
vilabu vya waandishi wa habari Tanzania
(UTPC) umebaini kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa na mtazamo tofauti juu ya mpango
huo huku wengi wao wakitaka
kulipwa wanapokwenda kutoa damu.
Sara
Kalinga mkazi wa Kihesa Iringa
amesema kuwa kwa upande wake amekuwa gizani juu ya mpango huo na kuwa kuna haja ya elimu
zaidi kuendelea kutolewa ili wananchi waweze kujenga utamaduni
wa kujitolea damu ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa damu salama katika benki ya damu.
Huku Joseph
Ndelwa akidai kuwa serikali inapaswa
kuweka utaratibu wa kuwalipa fedha wananchi wanaojitolea
damu ili kuhamasisha zaidi wananchi kuchangia mpango huo wa damu
salama.