Sunday, November 25, 2012

MILANGO YA KATAVI YAFUNGUKA .....

DKT GHARIB BILAL AZINDUA UWANJA NDEGE WA MPANDA NA KONGAMANO LA TATHMINI YA UWEKEZAJI UKANDA WA ZIWA TANGANYIKA

 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Gharib Bilal na Mkewe mama Aisha Bilal wakishuka kwebye ndege mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda mkoani Katavi kwa ajili ya uzinduzi wa mkoa mpya wa Katavi unaofanyika mjini mpanda kesho, Makamu wa Rais pia amezinddua uwanja wa ndege wa Mpanda na kuzindua Kongamano la Tathimini ya Mkutano wa Uwekezaji Ukanda wa Ziwa Tanganyika  uliofanyika Oktoba 17 mwaka jana na kushirikisha mikoa mitatu ya Rukwa, Kigoma a kufanyika mjini mpanda ambapo  sasyamekuwa makao makuu ya Mkoa wa Katavi.
 
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akisalimiana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda, kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe na katikati ni mama Tunu Pinda.
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal kushoto akijadiliana jambo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati wa Kongamano la kutathmini Mafanikio na Changamoto baada ya mkutano wa Uwekezaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika Kigoma na Rukwa uliofanyika Oktoba 17 mwaka jana mjini Mpanda
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza katika uzinduzi wa Uwanja wa ndege wa Mpanda, kshoto ni Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal na kulia ni mama Zakia Bilal.
 
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akizungumza wakati wa uzinduzi wa  uwanja wa ndege wa Mpanda mkoani Katavi leo mchana.
 
Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar Chambo akitoa taarifa ya ujenzi wa uwanja huo kwa Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal wakati wa uzinduzi mjini mpanda leo.
 
Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt. Charles Tizeba akimkaribisha Makamu wa Rais ili kuongea na wananchi wakati wa uzinduzi wa uwanja huo mjini Mpanda leo
 
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa uwanja wa ndege wa Mpanda baada  ya kukamilika kwa ujenzi wa uwanja huo, kulia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda na Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt. Charles Tizeba, kushoto ni Mama Zakia Bilal mke wa Makamu wa Rais.

 Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye, Dkt. Mary Nagu Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji Ofisi ya Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda Mke wa Waziri Mkuu na Mama Zakia Gharib Bilal Mke wa Makamu wa Rais wakiwa katika uzinduzi huo 
Makamu wa Rais akisalimiana na Mary Nagu Waziri wa Uwekezaji na Uwekezaji mara baada ya kuwasili mjini Mpanda leo Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Katavi Mselem na kutoka kulia ni Mbunge wa Mpanda mjini CHADEMA Mh.Said Arfi na Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt Charles Tizeba.
 
Makamu wa Rais Dkt Gharib Bilal akivishwa skafu na vijana wa chipukizi mjini Mpanda mara baada ya kuwasili mkoani Katavi leo.
 
Makamu wa Rais akisalimiana akipungia mkono wananchi waliofika kumlaki kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda mkoani Katavi leo, kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt Rajab Rutengwe na kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa Bw. Mselem.