Thursday, November 22, 2012

KUCHANGIA DAMU NI KUOKOA MAISHA YA WATU


 Wanahabari  wakiwa katika mafunzo ya uandishi wa habari za afya
HOSPITALI ya mkoa wa Iringa ilivyojipanga kukabiliana na tatizo la upatikanaji  wa   damu  salama kupitia mpango wa Taifa  wa damu salama.

Ikumbukwe  kuwa damu ni moja kati ya mahitaji muhimu katika mwili wa binadamu awaye  yeyote ili aweze kuishi ni lazima kuwa na damu ya kutosha mwilini mwaka.
Hospitali na vituo vya afya vya umma na binafsi ila bado uelewa wa baadhi ya wananchi katika kujitolea kutoa damu limekuwa ni tatizo kubwa kutokana na jamii kutokuwa na utamaduni wa kufika katika banki  za damu kwa ajili ya kutoa mchango wa damu.

Tayari  serikali  kupitia  wizara ya afya na ustawi wa jamii imekwisha  toa mwongozo wa damu salama kama njia ya kujipanga kuboresha  huduma  hiyo .
Lengo la kutoa mwongozo kwenye uundwaji wa kupangwa vizuri huduma kuongezewa damu, sambamba na Azimio la Afya Duniani Bunge WHA 28.72 (iliyopitishwa Mei 19, 1975) kwamba linataka nchi wanachama wote wa kuendeleza  uratibu wa kuongezewa damu ni huduma ya msingi na  hiari
Pia kupangwa vizuri Damu  (BTS) ni sehemu muhimu ya mfumo wowote wa afya kujifungua ili kufanikisha mpango huo mkakati madhubuti kwa ajili ya Usalama wa Damu inahitajika
Kutoka 2003 hadi 2007, Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Marekani  imefanya ukarabati wa vituo 7   vya kanda ambapo shughuli za mpango wa damu  salama umetekelezwa.
Vituo hivi kanda (ZC) ambayo ni ya kijiografia aitwaye ni Ziwa (Mwanza), Kaskazini (Moshi), Magharibi (Tabora), Mashariki (Tabora), Kusini (Mtwara), na nyanda za juu Kusini  (Mbeya) na Zanzibar.
Meneja  wa maabara ya mkoa wa Iringa Kimea Myefu amesema  kuwa katika  kutekeleza mpango huo na kuona kuwa  Hospitali ya mkoa  wa Iringa haipungukiwi na akiba ya damu  salama katika benki yake imekuwa na mpango maalum wa kupata damu salama kwa kutenga bajeti maalum ya kusafirisha damu kutoka Mbeya .
Myefu  amesema  kuwa  kutokana na mpango makakati huo  wa  kutenga bajeti ya kusafirisha damu  kwa  kiasi tatizo la damu katika benki ya damu  salama Hospitali ya mkoa  kutokuwa tatizo sana.
Hata  hivyo amesema  kuwa mwamuko kwa jamii katika  kujitolea  damu  katika mkoa  wa Iringa umekuwa mkubwa  zaidi  ukilinganisha na miaka ya nyuma kabla ya  kuanzishwa mpango  huo  wa damu  salama .
Myefu  amesema  kuwa idadi  kubwa ya  wananchi wanaofika  kuchangia damu tayari  wana elimu  juu ya mpango huo na wanajua afya  zao ila wale  wasiojua afya  zao ndio wamekuwa nyuma kujitokeza  kuchangia  damu.
“Kwa  sasa idadi kubwa ya  watu  wanaojitokeza  kuchangia  damu  zao wamekuwa wakichangia damu ila idadi ndogo hasa  wale ambao ni  wageni kabisa katika kuchangia  damu ndio ambao  wamekuwa  wakiondoka bila kuchangia  damu  kutokana na kutokuwa na uhakika  wa afya  zao”amesema Myefu
Kuwa  imeendelea  kutolewa na wananchi wengi  wamekuwa  wakijitokeza  kuchangia  damu na kati ya  watu  10 wanaofika  kutoa damu ni wawili ama mmoja pekee ndie ambae amekuwa akirudi pasipo kuchangia damu kutokana na matatizo ya  kiafya.

Aidha amesema  kuwa kuna haja ya jamii kujenga utamaduni wa  kuchunguza afya  zao mara kwa mara ili pale ambapo mchango  wao wa damu utahitajika basi  kuweza  kufika katika katika benki za damu na kuchangia damu.

Akielezea kuhusu utaratibu  wa mchangiaji  wa damu  Myefu amesema  kuwa kwanza ni lazima  kupimwa H.I.V , homa ya ini , magonjwa ya zinaa kama kaswende na mengine ,kiasi  cha damu alichonacho mchangiaji  pamoja na matatizo ya presha ,Kwani amesema kitaalam mwenye  kuchangia damu ni lazima awe na uzito  wa kuanzia  kilo 50 na kuendelea.

Akielezea  kuhusu mahitaji ya kawaida ya damu katika Hospitali  hiyo ya mkoa kwa  siku  kuwa ni uniti 8 na kuendelea  wakati akiba ya damu  iliyopo kwa  sasa ni uniti 25 ambacho bado kidogo ukilinganisha na mahitaji halisi ya  siku.

Hivyo ameiomba jamii kujenga utamaduni  wa  kujitolea  kuchangia  damu mara kwa mara  ili  kuboresha  zaidi  huduma  hiyo .
 Myefu amesema  kuwa baadhi ya  wananchi  wanaofika  kuchangia  damu kwa ajili ya  wagonjwa  wao wamekuwa  wakiamini  kuwa damu wanayochangia ni kwa ajili ya  matumizi ya wagonjwa  wao jambo ambalo halina ukweli  wowote.

“Kimsingi kama kuna mgonjwa anahitaji damu na ndugu  wakajitolea  kuchangia  damu damu hiyo haiwezi  kutumika kwa wakati  huo kwa ajili ya mgonjwa wake isipokuwa atapewa damu nyingine ambayo imetoka kituo cha damu  salama cha kanda kilichopo mkoa  wa Mbeya na si vinginevyo”
Kwani amesema kuwa damu inayochangiwa na katika Hospitali ya mkoa haitumiki hadi ipelekwe katika kituo cha kanda kwa ajili ya kuihakiki ubora  wake.
Pia amesema kuwa damu imekuwa na matumizi makubwa  hasa pale inapotokea ajali na majeruhi kufikishwa katika hospitali  hiyo.

Myefu amesema kwa mchangiaji wa damu hakuna malipo  yoyote  zaidi ya kupongeza kwa neon la ahsante na  kuwa hakuna biashara ya damu inayofanyika katika Hospitali  hiyo.

Wakati Hospitali  hiyo ya mkoa  wa Iringa ikiwa na mkakati  huo wa kuboresha  zaidi  mpango huo wa damu salama uchunguzi  uliofanywa na wanahabari wanachama  wa klabu ya  waandishi wa habari mkoa  wa Iringa (IPC)  wanaopatiwa mafunzo ya uandishi wa habari za afya chini ya ufadhili wa umoja  wa vilabu vya  waandishi wa habari Tanzania (UTPC) umebaini kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa na mtazamo tofauti  juu ya mpango  huo huku wengi  wao wakitaka kulipwa  wanapokwenda  kutoa damu.
Sara Kalinga mkazi  wa Kihesa Iringa amesema  kuwa kwa upande  wake amekuwa gizani  juu ya mpango huo na kuwa kuna haja ya  elimu  zaidi  kuendelea  kutolewa ili wananchi waweze kujenga utamaduni wa kujitolea damu ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa damu  salama katika benki ya damu.
Huku Joseph Ndelwa akidai  kuwa serikali  inapaswa  kuweka utaratibu wa kuwalipa fedha wananchi  wanaojitolea  damu ili  kuhamasisha  zaidi wananchi  kuchangia mpango  huo wa damu  salama.