Wednesday, November 21, 2012

TOSAMAGANGA HOSP YAPATA NEEMA

JAPANI YATOA ZAIDI YA MIL. 185 KUSAIDIA HOSPITALI YA TOSAMAGANGA
 Hili ndilo Kanisa katholiki la Tosamaganga- (Maana ya "Tosa Maganga, ni Tupa mawe,  ni Lugha ya kabila la Wahehe).
Uongozi wa Hospitali na Ubalozi wa Japan Wakitia sahihi mkataba wa Makubliano ya ukarabati wa Hospitali ya Tosamaganga, Iringa jana.
Barozi wa Japan, Bw. Masaki Okada akisain mkataba wa ukarabati wa Hospitali teule ya Tosamaganga, iliyopo mkoani Iringa.
 Mganga mfawidhi wa Hospitali Teule ya Tosamaganga Sister Sabina Mangi, akikabidhi zawadi ya kinyago, kwa balozi wa Japani Bw. Masaki Okada.



 Wauguzi wa Hospitali Teule ya Tosamaganga na baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Wilya ya Iringa, wakiwa na Barozi wa Japani Bw. Masaki Okada, katika picha ya pamoja.
 Sister Sabina Mangi, akiwa na Mkurugenzi wa hamashauri ya Wilya ya Iringa Bi. Pudensina Kisaka (Katikati) na mganga mkuu wa Wilaya ya Iringa, wakati barozi wa Japan, alipotembelea Hospitali ya Tosamaganga, kwa lengo la kuingia makubaliano ya kuifanyia ukarabati Hospitali hiyo.
  Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Tosamaganga,  Sister Sabina Mangi akitoa maelekezo kwa Balozizi wa Japan na wageni waliofika Hospitalini kwake.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Mh. Steven Mhapa akimkaribisha barozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaki Okada, katika ukumbi wa Hospitali teule ya Tosamaganga
Na Oliver Richard - Iringa
ILI kupunguza changamoto katika sekta ya afya, Ubarozi wa Japan nchini Tanzania, umesaidia ukarabati wa majengo katika Hospitalia Teule ya Tosamaganga, iliyopo Wilaya ya Iringa, baada ya Hospitali hiyo kuwa na changamoto kubwa ya uchakavu wa majengo.

Akiweka saini ya makubaliano ya mradi utakaogharimu US$ 123, 339, zaidi ya shilingi Milioni 185, barozi wa Japan Masaki Okada amesema mpango huo umekuja baada ya Ubarozi kutambua tatizo la Hospitali hiyo kuwa  na majengo chakavu, kutokana na kujengwa tangu mwaka 1970.

Masaki amesema mpango huo upo chini ya mradi wa Assistance for Grassroots human Security Projects, utakaokarabati wodi tatu za Hospitali ya Tosamaganga Hospitali ya Tosamaganga kwa sasa imezeeka huku majengo yake yakiwa hayaendani na hadhi yake ya kuhudumia wagonjwa.

Okada amesema mategemeo yake ni kuwa mradi huo utatekelezwa kikamilifu na kutasaidia kutoa huduma bora kwa wagonjwa wengi zaidi katika mazingira mazuri, na kuwa Hospitali tayari imepata wataalamu wa shirika la JICA kupitia “Project for Strengthening Development of Human Resource for Health”.


Mganga mkuu wa Wilaya ya Iringa Dr. Ignus Mlowe amesema changamoto kubwa inayoikabili Hospitali hiyo ni uchakavu wa majengo, hasa kwa wodi ya akinamma, wodi ya kuzalia (Matenity) na wodi ya watoto, kwani majengo mengi hayana muonekano wa kuridhisha.